
Content Marketing ni nini?
“Content Marketing” ni aina ya kujitangaza ambapo unakuwa unaandika taarifa za muhimu na zenye thamani kuhusu mambo mbalimbali yanayohisiana na biashara au huduma unayotoa.
Kiasi kwamba watu watakavyokuwa wana-search Google watakutana na ujuzi wako.
Na hivyo watakutafuta uwape huduma. Maana tayari utakuwa umewaonesha kuwa unajua unachokifanya kwa kupitia posti ulizo ziweka kwenye tovuti yako
Mfano: Kama wewe ni Bwana shamba, basi unaweza kuwa unaandika ujuzi wa kitaalamu kuhusu mambo tofauti tofauti yanayohusu kilimo chenye tija, fursa za kilimo na utaalamu wowote wa kudhibiti magugu na wadudu kwenye mimea mbalimbali na namna ya kulima aina mbalimbali ya mazao.
Taarifa hizo unaziweka kwenye tovuti yako. Kiasi kwamba hata kama unacho kitabu watu wasoma baadhi ya vitu kwenye tovuti yako na baadaye watakutafuta ili wanunue kitabu au wakulipe ili uwape utaalamu wako.
Na mitandao ya kijamii pia kama unaandika ujuzi wenye thamani na kuugawa kwa watu hiyo inaitwa “Content Marketing”
Mfano: Kuna Mwenzangu mmoja (Mwl. Salanga) anafanya vizuri sana Youtube . Yeye ni mtaalamu wa kutengeneza sabuni na bidhaa nyingine mbalimbali za kijasiriliamali.
Sasa huyu jamaa yeye anaandaa Youtube video, anajirekodi anafundidha namna ya kufanya.https://www.youtube.com/@mwalimusalanga/featured
Lakini mwishoni anauza yale malighafi zinazohitajika, na vitabu vinavyoeleza kwa mpangilio hatua kwa hatua. Na amekuwa na subscribers wengi .
Unaona hiyo?
kwa kuweka video za mafunzo mtandaoni amefanya wale wanaozitazama wamuamini, maana ameonesha kuwa anajua anachokifanya, na hao waliomwamini wanageuka kuwa wateja.
Na wengine wanambembeleza awauzie hizo malighafi ili nao watengeneze kama walivyoona anafanya.
Vivyo na WhatsApp pia. Anafundisha wateja kwa kutumia WhatsApp.
Anaunda WhatsApp groups kwa ajili ya madarasa mbalimbali anayoanzisha kwa ajili ya kufundisha namna ya kutengeneza bidhaa mbalimbali.
(Najua sio kila mtu anaweza kufanya youtube au kuandika kitabu au vipeperushi. Lakini unaweza kuwa na tovuti na unaweza kuwa na akaunti za mitandao ya kijamii. Ila wewe tafauta namna yako bora na njia yako bora ya kufanya “Content Marketing”)
Kama huwezi kufanya “Content Marketing” kwa njia kubwa kubwa basi fanya hata kwa njia ya WhatsApp Status basi.
_________
Leave a Reply